Sista Jo Anne Kelly anazungumzia kuhusu malezi ya MMM

Malezi kwa ajili ya Misioni

Na Sister Jo Anne Kelly MMM

Siku hizi, binti anayependa kujiunga na MMM huwasiliana nasi kwa muda mrefu kabla ya kuja kuishi kwenye jumuiya. Sista Jo Anne Kelly, aliyepata kuwa mmoja wa Wakurugenzi wa Wito wa MMM huko Nigeria, na ambaye ameshiriki katika kazi ya Malezi kwa Misioni kwa zaidi ya miaka 30, anasema kipindi hiki huchukua takriban mwaka mmoja. Wengi kati ya wana MMM kutoka Nigeria ambao pia ni Wamisionari kwa namna yao wamepata kuonja malezi ya Sista Jo Anne katika hatua moja au nyingine katika safari yao.

jo_anne_kelly1aKatika hatua za mwanzo za maandalizi, binti hupata fursa ya kutujua nasi kumjua. Hi hufanyika kwa njia ya barua na kutembelea jumuiya yetu. Kwa kawaida hutukaribisha nyumbani kwao na mahali penginepo anaposoma au kufanya kazi. Binti anapochagua kufuata maisha ya MMM, ni uchaguzi wa kuwa katika shirika hili kama familia anayoipa kipaumbele. Japokuwa kwa kufanya hivyo hakumtenganishi na familia yake asilia, mara kwa mara tunawasaidia wazazi kutambua uchaguzi unaofanywa na binti yao. Nao pia wanapaswa kusaidiwa kuona kuwa maisha yetu yananahusika na kufanya kazi katika sehemu zisizo salama, zenye uwezekano wa hatari, wakati mwingine kwenda katika maeneo yaliyokubwa na vita au sehemu zisizo na utulivu.

Eneo jingine ambalo ni muhimu kwa familia za Afrika ni kuwasaidia wazazi kutambua kuwa kama wamisionari, tunazikwa mahali tulipofia. Mara nyingi tunasistiza kuwa tunaishi kinyume na utamaduani na hivyo baadhi ya familia huona vigumu kukubaliana na jambo hili kwa kuwa ni kinyume na mila zao.

MMM sio maisha rahisi!

Kama binti bado anapenda kujiunga nasi, atahudhuria mafungo pamoja na wengine ambayo yatakuwa na msisitizo juu ya mfumo wa maisha wa MMM. Katika mafungo hayo, baadhi ya Masista wakubwa wa MMM, na baadhi ya wale vijana walio katika programu ya malezi hushiriki ili kusaidia. Pale mhusika na mkurugenzi wa wito anaporidhika kuwa ni tayari, hufanyika utaratibu wa mahojiano na jopo maalum. Pengine baadhi wanaweza kuona hii kama kujaribiwa. Mfumo wa maisha ya MMM sio rahisi, na hivyo tunajitahidi kuwasaidia wakandidati kuelewa hili tangu awali. Mhusika ataombwa kuleta ripoti ya hali ya afya yake na tathmini ya kisaikolojia ya hivi karibuni. Haya ni kati ya yanayohitajika ili kujiunga na mashirika mbalimbali siku hizi. Wengi wanaofikia hatua hii kwa njia moja au nyingine hawaendelei.

Ni dhahiri kuna tofauti kubwa kati ya ulimwengu na mfumo wa maisha ya mabinti wa leo na ule wa miaka yangu ya mwanzo katika kazi hii. Nilipoanza kulikuwa na nidhamu kubwa katika familia, mfumo uliokuwa na usalama zaidi, na kulikuwa na matatizo machache ya kimaadili katika jamii. Kwa leo inakuwa vigumu kwa vijana kujua hasa ni kwa ajili ya nini wanataka kutoa maisha yao. Hivyo, kufanya mang'amuzi ya wito ni muhimu sana. Tunajitahidi kuwasaidia kung'amua kama kweli wanataka kuyatoa maisha yao kwa Mungu, au kama wanatafuta aina Fulani ya usala katika maisha, au pengine wanatafuta fursa ya kupata elimu n.k. Nafikiri yeyote anayechagua maisha ya kitawa kwa leo ni mwanamke jasiri, kwa sababu anapaswa kuwa tofauti na wenzake katika mfumo wa maisha, matarajio na matamanio.

Tunachohitaji toka kwa mabinti wanaotaka kujiunga nasi ni kujitoa kwao kwa Kristu, kiasi fulani cha uelewa wa utume Kristu na mvuto kwa utume wa MMM - ambao ni Utume wa Uponyaji. Tunaangalia hali ya kuvutwa kwa utume huu walau kwa kiasi Fulani. Binti anapaswa kuonesha uelewa kwa kiasi fulani, pia moyo wa sadaka, kuwa mfumo huu wa maisha unaambatana na kuachana na mambo mengi.

Tunahitaji mtu ambaye ni mwenye furaha, na mwenye uhuru wa kutosha kufanya uamzi huu. Hata hivyo anapaswa kukua katika uhuru huu. Programu yetu ya malezi ya awali inahusiana na mambo haya.

Nini kinafanya MMM wavutie?

Unaweza kustaajabu juu ya nini kinawavuta mabinti kutoa sadaka hii leo. Nini hasa juu ya MMM kinachofanya wavutiwe na maisha yetu?

Kwa mara nyingi wito umekuwa fumbo. Vijana ni wakarimu na wanataka kuyatoa maisha yao kwa ajili ya Mungu na wengine. Wana hamu ya kuwasaidia wale ambao hawakubahataika maishani. Wengi hawapendezwi na hali ya ulimwengu kama unavyoonekana - jinsi fukara walivyo maskini, na jinsi kulivyo na mahangaiko - hivyo wanataka kuleta mabadiliko. Wanaona kuwa MMM inawapatia fursa kujihusisha na hili kikamilifu.

Huko Nigeria, mabinti wanapokuja kwenye jumuiya yetu, wanatoka kwenye utamaduni wenye uelewa wa Kanisa na utamaduni wao. Katika mwaka wa kwanza wa programu ya malezi, tunaanza kuona juu ya maendeleo ya mwanadamu, makuzi ya mtu binafsi, tukitumia maandiko matakatifu kwa njia tofauti na jinsi walivyozoea, na pia tunajifunza jinsi ya kuhusiana na Mungu kwa njia tofauti, hii inabadilisha mtazamo wao mzima - wakati mwingine juu chini. Wanaonekana kupata mtazano mpya juu ya ulimwengu, Mungu na wao wenyewe.

Shauku

Katika mwaka wa kwanza, kwa kawaida kuna shauku kubwa, furaha ya kuvumbua yote haya. Siwezi kuielezea shauku hii. Ni kana kwamba kila mmoja anajifunua kwa kitu ambacho ndani yake hakutarajia. Nikizungumzia kwa mapana sio rahisi kuelezea. Yaani hapa anajifunua kwa njia ya pekee kwa Mungu, kwa nafsi yake na kwa watu wengine pamoja na mahitaji yao. Hili hutokea kwa kila mmoja kwa njia tofauti na kwa kiwango tofauti na wakati mwingine kunakuwepo juhudi kubwa na maumivu ili kufikia hali hiyo. Hii inadai tafakari kubwa na kuyatazama maisha, kuangalia kinachoendelea katika nafsi yako, katika kila siku, kwenye maandiko matakatifu, na katika kile Kristu ananena na kutenda kwa maisha ya kila mmoja.

Pindi wanapojiunga na jumuiya, mabinti hutwaa jukumu la usimamizi wa nyumba, mahesabu, manunuzi, kupika, utunzaji wa nyumba, ukarabati na shamba. Pia wanakuwa na muda wa kutosha kushughulika na utume, katika moja ya hospitali zetu, zahanati au sehemu nyingine inayohusiana na kazi zifanywazo na MMM. Hii huwaweka karibu na watu fukara na wenye ina mbalimbali ya uhitaji. Pia inawapatia fursa kutafakari juu ya uzoefu waupatao na kinachotendeka ndani yao.

Pia pana kazi katika vikundi. Hii inahusisha kujifunza juu ya masomo kama sala, masomo ya kiroho, maandiko matakatifu, katekesi ya msingi na elimu ya Kikristu katika kukuza imani na uhusiano wao na Mungu. Mbali na hayo hujifunza juu ya maisha ya kitawa, historia ya MMM, na kupata uelewa wa karama yetu na changamoto za kimisionari tunazokabiliana nazo.

Kazi katika kikundi pia inajumuisha tathmini ya rika. Katika kipindi cha programu ya malezi vijana hujifunza kukabiliana wao kwa wao na kusikiliza yanayozungumzwa toka kwa kila mmoja. Pia kila mmoja hupata fursa ya kujifanyia tathmini. Akinamama hawa watakuwa viongozi katika majukumu watakayopewa baadaye. Katika malezi ya awali kila mmoja huvumbua viongozi asilia na pia anahitaji kuwatia moyo wengine. Kila mmoja ana kipaji cha uongozi. Kwa upande wangu, ushiriki wangu kwa hili umekuwa wa kustaajibisha; na zaidi ya yote umenipa changamoto ya kuishi kile ninafundisha. Hakika hii kwangu imekuwa zawadi kubwa kwa makuzi yangu.

Search...