Hatua za kuwa Sista wa MMM

Hatua ya kwanza kuelekea kuwa Sista wa MMM, ni kumtafuta Mkurugenzi wa Wito aliyekaribu nawe. Kama unapenda kujua tafadhali wasiliana nasi, tujulishe uko nchi gani nasi tutakutambulisha kwa Mkurugenzi wa Miito aliye karibu nawe. madeleine-a1

Kisha kuwa na mawasiliano na Mkurugenzi wako wa Wito kitafuata kipindi ambapo atakusaidia kung'amua na kupambanua wito wako. Kama wote mtakubaliana kuwa MMM ni sahihi kwako, utaandaliwa utaratibu wa kufanyiwa mahojiano. Katika picha kulia ni Sista Madeleine Le Blanc, Mkurugenzi wa Wito huko Marekani. Kama unaishi Marekani au Kanada mtumie barua pepe kwa anwani hii This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

ugwuliri_teresaHatua inayofuata ni ya Upostulanti, ambayo huchukua kipindi cha miezi michache mpaka mwaka mmoja au zaidi. Sehemu ya kipindi hiki inatoa fursa ya kuishi katika Jumuiya ya Masista waprofesi wa MMM. Katika picha kushoto ni Sista Ugwuliri. Baada ya miaka mingi ya utume nchini Malawi, sasa amerejea Nigeria ambapo anashughulikia jumuiya ya wapostulanti nchini humo wanaojifunza juu ya maisha ya MMM pamoja na changamoto watakazokabiliana nazo katika safari yao.

Hatua ya pili kwa mpostulanti anayependa kuendelea Novisiati. Mwaka wa kwanza hujulikana kama Mwaka wa Kiroho. Hiki ni kipindi cha kuzama katika sala na kujifunza historia na karama ya shirika la MMM na ya Utume wa Kanisa Ulimwenguni.

Katika mwaka wa pili wa Unovisi, maisha haya ya sala na masomo huunganishwa na kujipatia uzoefu halisia kwa kufanya utume kati ya watu fukara. Kwa kawaida Unovisi hujuimuisha ushiriki wa wahusika katika kujifunza katika kundi linalojumuisha mashirika mbalimbali. Hii ni fursa nyingine ya kutafakari na kujifunza katika mchanganyiko wa wanashirika wake kwa waume wa mashirika mengine, na hivyo kuwapatia stadi za kujitambua, maendeleoa ya mwanadamu, na mang'amuzi ya kina ya kiroho na maisha ya utume.

dervilla_crop1Kwa sasa tuna Novisiati mbili, moja iko Nairobi, nchini Kenya, na nyingine Ibadan, nchini Nigeria. Hata hivyo Malezi yetu yanafanyiwa mapitio.

Miaka michache iliyopita tuliwauliza Wasimamizi wa kila Novisiati watueleze Nani huthubutu kuwa mwana MMM? Walitujibu kwa maneno yenye changamoto. Ukitaka kusoma majibu yao, Bonyeza hapa. Sista Dervilla O'Donnell, pichani kulia ni mmoja wa waandishi wa tafakari hiyo.

Hatua ya tatu hufuata baada ya kumaliza Unovisi na kupata tathmini na ripoti nzuri. Hapa Sists huweka Nadhiri za Kwanza. Nadhiri hizi ni za muda ambapo Sista atarudia ahadi kila mwaka. Wakati wa kipindi hiki cha nadhiri za muda, Masista hutumwa kwa moja ya maeneo ya utume wetu. Wakati mwingine baadhi wanaweza kuamua kuwa maisha ya uSista wa MMM sio chaguo lao sahihi. Wengi wa walioacha njia hii hujisikia walichojifunza ni cha thamani na hivyo hubaki marafiki wa karibu wa MMM hata kama maisha huwaelekeza kwingineko.

 

Search...