Nani anathubutu kuwa Wamisionari wa Tiba wa Maria

Nani huthubutu kuwa mwana MMM?

unamah-c1Swali hili tunamwuliza Sista Bernadette Unamah (kulia) na Sista Dervilla O'Donnell (chini), kipindi walipokuwa wanashughulika na Novisiati zetu mbili zilizojumuisha watu wa tamaduni mbalimbali, ambapo mabinti wanaojiunga na MMM leo huongozwa kuchagua MMM kama njia ya maisha.

Kuhusiana na kinafomfanya mtu awe mwana MMM, Sista Bernadette Unamah anajibu bila kusita: "Unapaswa kuwa kweli mwanadamu na mwenye nidhamu kati ya jamii inayoangalia zaidi mali. Kwa mwanamke wa kiNigeria, wewe si kitu kama hauna fedha, watoto na mji wako. Kwa hiyo moyo wa sadaka, nidhamu na kujitoa kwa nadhiri za maisha ni mambo ya wanaothubutu kuwa hivyo."

Anayethubutu kuwa mwana MMM ni mtu anayehiari kugusa ukweli juu ya utambulisho wake kama mwanamke, mnyonge, fukara na wakati huohuo ni tajiri kwa namna tofauti. Ni Yule anayehiari kuhatirisha, kutumainia neema za Mungu na uwezo wake mwenyewe. "Huyu ni Yule anayejitahidi kuwa wazi katika kupenda na kupendwa, mwenye moyo kwa ajili ya watu na wenye kushikamana na maskini na waliotengwa."

"Kuwa mwana MMM inabidi uwe mtu aliye tayari kujifunza na kufunzwa, kujiendeleza mwenyewe na kusoma alama za nyakati zetu ili kuwa nabii wa kesho. Anapaswa awe mtu anayeweza kusimama peke yake, anayeweza kujitegemea pasipokuwa mbinafsi."

dervilla_on_the_ladderSista Dervilla anaongeza: "Ningetafuta wanawake wanaoishi tunu za ukarimu na utayari, wanawake wasio wabinafsi bali waliomweka Mungu katikati ya maisha yao - wanawake wanaojisikia kuwa wameitwa kwenye njia ya maisha ya kimisionari na wanaovutwa na utume wa Kristu wa uponyaji. Wanahitaji kuwa tayari kuhatirisha na kuheshimu watu wote."

UNAWEZAJE KUELEZEA MAISHA YA NADHIRI KAMA MWANA MMM?

Kadiri ya Bernadette, maisha ya nadhiri kama mwana MMM yanatoa changamoto kwa vijana kujenga moyo wa kushirikishana, kupekea na kutwaa majukumu kwa ajili yako na wengine. Maisha yanawapa changamoto kujifunza kuwa kimya na kuwa tayari kwa ajili yaw engine katika ulimwengu ambao ni wa makelele, wenye sughuli nyingi na ubinafsi. Katika jamii iliyovurugwa na vita, chuki na umasikini, MMM kama njia ya maisha inatoa upendo patanishi na kuleta matumaini kwa wale wasio na matumaini. Katika ulimwengu ambao watu wanajari zaidi vitu si rahisi kujitoa, vijana wanapendelea zaidi mambo ya muda mfupi. Maisha ya nadhiri yanatoa changamoto kwa ulimwengu kutazama uaminifu, kujitoa, udumifu, sadaka na ujinsia. Nni mwaliko kwetu kushirikiana na Mungu kuwawezesha watu kutumia vipaji vyao kutengeneza mazingira mazuri ya kuishi.

Dervilla anasema: "Nakubaliana na Bernadette. Tunaishi katika ulimwengu unaobadilika haraka, ambapo unahitaji wa vitu kwa wakati huu. Tunaaminishwa kuwa vitu hivi vitatupatia furaha, ambapo mahusiano yamevurugwa na kujitoa ni kwa muda mfupi. Pamoja na mtazamo huu kuna kutafuta maana na kuridhika. Nadhiri ya useja, nadhiri ya kupenda, ni nadhiri inayowashangaza watu wengi. Tunawezaje kuiishi na kuchagua kutoluwa na kaya zetu wenyewe, familia na watoto? Katika jamii ambapo nguzu na mamlaka ya kisiasa vimejaa ufisadi, uelewa juu ya nadhiri ya utii kama nadhiri ya kushirikiana inatoa changamoto kubwa. Maskini katika jamii tunakotumwa wanatufundisha kutokana na umaskini thamani ya kushirikishana, maisha ya kawaida, uwajibikaji na umuhimu wa mahusiano. Kwa Manovisi na kwa kila mmoja wetu kuishi kikamilifu nadhiri hizi kunatudai kuchagua. Ni uchaguzi ambao mizizi yake ni uhusiano binafsi na Yesu na imani kuwa tunahusika katika kujenga Ufalme wa Mungu katika ulimwengu uliogawanyika vibaya."

MNAWAFUNDISHAJE WANOVISI KUSALI?

Sala pamoja na muunganiko na Mungu ni sehemu ya maisha ya Waafrika, kama walivyo waIrish, anasema Dervilla. Hali ya kutambua mambo ya kiroho ipo kama tukiitumia kwa kiwango hicho tambuzi. Wakati mwingine inategemeana na hali ya mtu ya kutafakari. Katika jumuiya, umetengwa muda kwa ajili ya sala za pamoja na sala binafsi kwa uangalifu; Wanovisi wanashirikiswa katika maadalizi ya liturjia kwa mwaka mzima. Aidha katika kozi mbalimbali kwenye Novisiati na katika programu zinazoshirikisha mashirika mengine, wanovisi hupata fursa ya kutosha kuchambua na kushirikishana mang'amuzi yao katika yale yanayofundishwa na waandishi maarufu wa mambo ya kiroho.

JE KIONGOZI WA WANOVISI ANAWEZA KUZUNGUMZIA KURIDHISHWA NA KAZI?

Dervilla anatuambia: "Huwezi kuwa na malengo ya kutimiza kama ilivyo kwa kazi nyingine." Anaendelea, "Ni Roho wa Mungu anayesimamia kazi hii mimi naalikwa kushirikiana na Roho huyu na sio kuwa kikwazo. Ninatambua mwaliko huu wa kushiriki katika maisha matakatifu ya Wanovisi, ambapo ninagusa Fumbo la Mungu linalojifunua kwa njia ya pekee kwa kila mmoja. Ninajisikia kubahatika na ninashukuru kuweza kuwasindikiza Wanovisi katika safari yao ya imani, kujitambua na kukua katika utambulisho wao pamoja na MMM." Kuridhika? Ndiyo. "Ni faraja iliyoje kuona mabinti hawa wakikuwa, kukomaa katika imani yao, katika kujitambua kuwa wao ni kina nani na utambulisho wao katika shirika la MMM. Ninapoona wakihiari kwa maisha ya kuwahudumia kwa huruma wagonjwa, au wasiojiweza, hii hunifanya nione kazi yangu ina thamani."

Bernadette pia anaongelea juu ya hali ya kutembea katika uwanja mtakatifu na juu ya vijana kutafuta utambulisho. "Hakika ni kutembea katika uwanja mtakatifu. Kazi ya kuwasindikiza mabinti katika safari yao ya kiimani wakati mwingine inaweza kuwa ngumu. Ni wajibu unaodai zaidi na hutumia nguvu lakini katika maisha yao kuna kitu hunitia nguvu. Ninaridhika pale ninapoweza kumpatia matumaini binti wakati wa jitihada zake kupata utambulisho. Inatia faraja kubwa unapomwona Mnovisi akikuwa hatua kwa hatua kuanzia pale alipoingia - wakati mwingine akiwa na hofu na kutojua anakoelekea, akiwa na shauku juu ya hamu yake ya kujitoa, kasha kumwona akielekea katika kipindi cha uhuru na kuwa mwajibikaji mwenye mtazamo chanya wa maisha."

NI KIPAJI GANI MUHIMU SANA KINACHOHITAJIKA KWA KAZI YAKO?

Uvumilivu, wote wanakubaliana. Wewe sio msimamizi mkuu bali ni Roho Mtakatifu anayeongoza haya yote, unapaswa kuwa na subira kwa muda wa Roho huyu. Ili uweze kushiriki kikamilifu na sio kuwa kikwazo kwa mwendo huo na kuzingatia mwenendo ndani ya kila mmoja ni changamoto kubwa. Patience, they both agree. Unapaswa kuwa msikilizaji mzuri, kuwa mwenye huruma, kuwa wazi kwa tofauti aidha za kiutamaduni au kuhusiana na nafsi ya mtu. tabernacle

Bernadette anasisitiza: "Kwa njia moja, Wanovisi ni vioo vyetu! Wananiangalisha nione nini kinapaswa kutendeka; kuwa mara kwa mara nahuisha imani yangu na kukumbuka juu ya yote yanayoambatana na maisha yangu ya nadhiri. Unapowaona mabinti hawa wazuri wakiwa na bidii na hamu ya maisha ya kitawa katika ulimwengu unaojali zaidi vitu na ushindani, hunikumbusha kuwa kuna mengi ya kustaajabia na kuthamini katika maisha ya kitawa." 

Dervilla anasema: "Moja kati ya mambo yenye changamoto kubwa katika utumishi huu ni mabadiliko endelevu ya uanajumuiya. Novisiati ni miaka miwili, hivyo uanajumuiya wetu hubadilika sana kwani Wanovisi huwa Masista waprofesi au kuondoka. Aidha pana utajiri mkubwa na Baraka katika hili kwani wanachama wapya hutoka mataifa na tamaduni tofauti. Ni mara chache napata fursa ya kukutana na Wanovisi wangu waliotangulia kwani hutumwa sehemu za mbali kwa utume. Hakika ninafarijika sana ninaposikia toka kwao katika utume mpya huko Brazil, Nigeria, Malawi, Uganda na jinsi wanavyopata changamoto katika maisha na uzoefu wanaopata na jinsi wanavyobobea katika kuelewa njia yetu ya maisha kama MMM."

Tabernakulo katika Kikanisa cha MMM Novisiati ya Nairobi.

Search...