Sista Marian Scena anazungumzia mapendeleo yake

Napendelea kuangalia ndege

Na Sista Marian Scena

marian_scena_tanzania1smMmoja wa masista wenzangu katika shirika la MMM aliniuliza, "Marian, kope zake ni rangi gani?" - hii ilikuwa kama kichekesho na utani ndani yake! Hata hivyo hakutambua kama ni kwa namna gani kope ni muhimu katika kumtambua ndege niliyekuwa namtazama. Hii humchanganya yule anayekuwa na wajibu wa kuangalia ndege!

Tangu nikiwa mtoto mdogo tulikuwa na kiota cha kulishia ndege nje ya dirisha la jiko letu na mama yangu alikuwa na mazoea ya kunionesha ndege wa aina mbalimbali waliofika hapo. Japo nilipendelea sana ndege lakini sikutilia maanani mpaka pale nilipokuja Tanzania ambapo uzuri na uwingi wa ndege unastaajabisha.

Mara nilipopata darubini kwa mara ya kwanza nilizama katika jambo hili! Mwaka 1991 nilikutana na wanandoa wawili toka Wales waliokuwa wanafanya kazi Singida ambao walinijulisha kwa familia ya kiingereza ya Liz na Neil Baker iliyoishi Tanzania, ambao walikuwa akiandaa Atlasi ya Ndege wa Tanzania. Nilipokutana nao walinielekeza juu ya utaratibu wa kutazama na kutoa taarifa ya ndege niliowaona kila mwezi. Hii ilimaanisha kuandika juu ya wapi nilipowaona, idadi yao, aina, na kama wanazaliana au la.

Watu wengine waliojihusisha na ndege kama mimi toka sehemu nyingine nchini, walitoa taarifa kila mwezi na taarifa hizi zilikusanywa kwa ajili ya kuandaa Atlasi hii ya ndege. Kujihusisha na ndege ni jambo la kufurahisha - kwa kuwa hakuna sababu nyingine isipokuwa kushangaa na kustaajabia viumbe marafiki wa Mungu. Hata hivyo kule kutoa mchango wangu katika Atlasi ya ndege inayoandaliwa unanipa motisha zaidi.

Nimegundua kama kushughulika na ndege ni ziada ya ajabu katika huduma yangu ya udaktari ambayo hudai umakini na hutumia muda wa kutosha. Hata nisipopata muda wa kushughulika na ndege, mwisho wa siku yenye shughuli nyingi huweza kuwaona ndege wa kila aina niwapo njiani kurudi nyumbani nikitokea hospitali.

Nafikiri kuwa daktari na kujijengea uwezo wa kuchunguza kwa kiwango cha juu imenisaidia kutazama hali mbalimbali za ndege ambazo ni muhimu katika kumtambua.

Naona kujihusisha kwangu na ndege ni kichocheo kikubwa katika sala zangu. Hakika ni kama sala; natumia muda kusubiri bila kujua kama na ni nini nitajua juu ya Mungu, lakini nashukuru kwa namna yeyote ambayo kwayo Mungu hunijia. Ninaposhughulika na ndege huwa kimya na mwenye subira, bila kuwa na hakika nitaona nini. Wakati mwingine sioni kitu kama jinsi mtu anavyoweza kukaukiwa katika sala. Lakini mara nyingi hushangaa pale ninapoona ndege mgeni kwa mara ya kwanza au tabia ngeni ya ndege. Mara kwa mara hujikuta namtukuza Mungu kwa ajili uzuri wa viumbe wanaonizunguka na uzuri walionao ndege. Sala na kuangalia ndege huenda pamoja.

Kila niendapo niko makini na hutafuta ndege. Hii hufupisha muda wa safari ndefu na katika barabara mbovu na kuifanya safari hiyo iwe ya kufurahisha. Japo huwa simwombi dereva kusimamisha gari ili niwatazame ndege wangu, lakini bado naweza kutambua asilimia 25 ya ndege ninaokutana nao katika safari.

Ninapokuwa na siku ya mapumziko, maramoja kwa mwezi, hupendelea kutembelea Bwawa la Mianji lililo karibu. Hii huchukua masaa matano hadi saba kutembea kwa makini na kwa mwendo wa tafakari. Katika siku hiyo huweza kuona zaidi ya aina hamsini za ndege katika eneo la Bwawa na kati ya aina kumi hadi kumi na tano njiani.

Mpaka sasa nimekwishaona aina tofauti 498 za ndege nchini Tanzania. Kati ya hao, aina 122 wamekuwa katika eneo Hospitali ya Makiungu au wamepita hapo. Ninastaajabia tofauti hiyo ya ajabu ya ndege hata nyumbani tunapoishi. Mpaka sasa bado sijapata muda wa kuweka idadi kamili ya aina zote za ndege niliowaona maishani katika nchini nyingine nilizofika.

tanzania_birds1Yeyote anayeweza kuona au kusikia anaweza kuwa mpenda ndege. Kwa mtu mwenye nguvu na anayependa kusafiri ataweza kuona zaidi. Lakini si lazima uwe mwenye afya njema! Hata yule ambaye hawezi kutembea bado atafurahia kuona na kuwasikia sauti za ndege. Hii inaweza kuwa jambo unalopendelea kwa muda au likawa la kila siku. Natumaini niamsha matamanio yako ya kutaka kugundua uzuri wa marafiki wa Mungu wenye manyoya.

Maelezo ya picha:

Starlings watatu. Wa katikati ni mdogo. Bado hajawa na macho ya dhahabu wala kuwa na mchirizi mweupe.

 

Search...