MMM na Njia ya Maisha ya Kibenediktini

glenstall_abbey_gateway1Mwaka 1934, Mwanzilishi wetu, Marie Martin, alikuwa na shauku kupata nyumba kwa ajili ya kundi dogo la wanawake walioonesha kuvutiwa na hamu yake ya kuanzisha shirika la kimisionari la masista. Alifurahishwa na wazo la kuwa wangeliweza kuwasaidia Wamonaki wa Glenstal waliokuwa wakikumbana na magumu mengi ya kijamii katika shule yao mpya ya bweni, hivyo kupata malezi ya kiroho kutokana na usaidizi wao.

Baba wake wa Kiroho, Padri Hugh Kelly SJ, alistaajabu endapo mafunzo ya kibenediktini yangeliweza kuleta mabadiliko kimtazamo ya kimonaki na kiliturjia, na kuona kuwa maisha haya ya kiroho yasingewafaa sana wao kama taasisi iliyopaswa kuwa kimsingi ya kitume.

founder_small1Marie alilitazama hili kwa hali tofauti kwa ujumla. Yeye aliweza kutofautisha kati ya roho na kuishi kwa matendo maisha ya kiroho ya kiBenediktini. Aliyasoma maandishi ya mmonaki na abate maarufu wa Ireland, Dom Columba Marmion. Alipenda aunganishe shirika lake jipya la kimisionari na mapokeo ya kiroho yaliyojaribiwa kwa karne nyingi. Roho ya Kanuni ya Mtakatifu Benedikto ingelitoa uhuru na wakati huohuo, kule kujitoa alikokuona ni muhimu kutimiza ndoto yake ya shirika la kimisionari la tiba. Kanuni hiyo ingeliweza kuingizwa kwa uangaligu katika Katiba ya MMM.

sr_m_patrick_leydonWakati Nora Leydon alipokutana na Marie Martin, alikuwa na umri wa miaka ishirini na saba; akitokea Kilmactranny, Co. Sligo, ambapo alikuwa akifanya kazi kama Karani wa Padri Patrick Whitney, wa Shirika la Kimisionari la Mtakatifu Patriki lililokuwa limeanzishwa.Tarehe 19 Machi 1934, Nora aliwasili Glenstal kujiunga na Marie, na hivyo ukawa mwanzo wa Shirika la MMM, ambalo lilianza rasmi miaka mitatu baadaye.

Kitambo kidogo baadaye, Bridie O'Rourke aliwasili Glenstal. Alipewa jina na kuwa Sista M. Magdalen ambapo alishughulika sana na kuitangaza kazi ya MMM mpaka alipozeeka. Alifariki tarehe 11 Novemba 2008. Mara kwa mara alisema ulikuwa ni mfano wa wamonaki uliomfurahisha zaidi ya Kanuni. Miaka kadhaa iliyopita aliandika juu ya Njia ya Maisha ya Kibenediktini: Ushuhuda Binafsi.

sr_m_immaculata_nicholsCarrie Nichols alizaliwa Dublin na kubatizwa katika Kanisa la Mtakatifu Paulo huko Arran Quay, parokia ambapo Dom Marmion alibatizwa – kama alivyotukumbusha mara kwa mara. Alikuwa na umri wa miaka kumi na nane alipotambua shirika tarajiwa la wamisionari wa tiba. Alijiunga kikundi kidogo cha waanzilishi huko Glenstal mwaka 1936. Alivutiwa sana na roho ya Mtakatifu Benedikto tangu akiwa kijana.

Jumuiya hii ndogo taratibu ilikua na kutoa msaada kwa Wamonaki kuanzisha Shule ya Bweni ya Wavulana ya Glenstal. Hapo tarehe 11 Februari 1936, Vatikano ilitoa hati ambayo Marie Martin alikuwa ameisubiri kwa takriban miaka ishirini. Tokea hapo watawa wanawake wamisionari waliruhusiwa, na kuhimizwa kujihusisha na tiba. Hatimaye mlango ulifunguliwa kuanzisha Medical Missionaries of Mary.

Ulikuwa ni wakati wa kutoka kwenye kiota cha kiroho kilichotolewa na Glenstal kwa shirika change la wamisionari. Baada ya miezi kadhaa, kundi hili dogo lilianza kujiandaa kwenda Afrika. Hata hivyo uhusiano kati ya Medical Missionaries of Mary na Monasteri ya Wabenedikitini ya Glenstal uliendelea kwa miaka yote iliyofuata.

Search...