Wito wa MMM

ahanonu_grace1Mwaliko wa kuwa mtawa wa shirika la Kimatibabu la Wamisionari wa Maria (MMM) unatoka kwa Mungu. Sheria zetu zinatueleza kwamba 'unaitwa kwa safari ya kipekee

Utume wetu ni safari ya kiimani inayotupeleka katika sehemu za mashambani duniani kote. Tukishakuwa pale, tunajaribu kuonyesha upendo wa Mungu kwa watu hasa kwa kazi ya uponyaji, kama vile Yesu alivyofanya akiwa duniani. Mhimili wa karisma yetu ya uponyaji unatambua kwa njia ya kipekee afya bora kwa kina mama na watoto.  

borda-mc_small1Hii kazi inaweza kufanyika katika mahospitali, zahanati au katika vikundi vya huduma ya afya vya parokia kati ya watu tuanoishi nao. Pamoja na masista ambao wamehitimu katika sanaa ya kiafya, utume wa MMM unahitaji masista ambao wamehitimu masomo ya teologia, usimamizi wa biashara, taaluma ya uenezaji wa habari nk. Hakuna talanta yeyote ambayo haifai katika kazi ya utume ya MMM.

Maisha yetu ya kiroho yamejengwa katika msingi wa itikadi za zamani za Mtakatifu Benedikto. Isipokuwa tunafanya kazi za kawaida duniani, tunajaribu kuishi maisha ya sala.

Mwongozo wa Kazi zetu: sisi kama MMM, katika dunia ambayo imegawanyika zaidi, sisi ni kinamama ambao tunawaka moto wa upendo wa Mungu wa uponyaji. Katika maumivu yetu na Kujitolea katika hali ya hatari, tunaenda kwa watu kutoka tamaduni tofauti, mahali ambapo mahitaji ya kibinadamu ni mengi zaidi. Uaminifu wetu katika uhusiano kati ya viumbe vyote vya Mungu unatusuhi kupokea uponyaji kwa ujumla na kufanya kazi ya maridhiano, haki na amani.

Mahali tulipo: Katika ukurasa wa mwanzo katika tovuti yetu, utapata orodha ya nchi ambazo jumuiya za MMM ziko. Sasa hivi kuna masista 400 wa MMM kutoka nchi 16.

Utajifunza mengi zaidi kuhusu maisha ya MMM kama utasoma majibu yetu ya maswali ambayo wamama wadogo hutuuliza sisi. Kama unajisikia kwamba Mungu anakuita kuwa MMM, unaweza kujifahamisha zaidi kuhusu hatua ambazo mtu hufuata katika safari ya kuwa MMM.

Unaweza kusoma zaidi kutoka kwa mkurugenzi wa miito wa MMM mwenye ujuzi, Sista Jo Anne Kelly

Wakurugezi wawili wa wanovisi wanajibu swali: Nani Anaweza kuwa MMM?

Wasiliana nasi na utuulize maswali. Tutafurahi sana kusikia kutoka kwako! Na utapata jawabu yako binafsi.

donors_skydiversSio kila mtu ameitwa kuwa sista. Mungu huwaita wengine kwa njia tofauti hili wawajibike katika familia. Sio lazima kuruka na parachute ili uchangishie hela kama Chris Hemsley alivyofanya. Kila mwanchama wa familia ya MMM wana namna yao ya kipekee ya kuhusika - na kila mmoja analeta tofauti. Na wewe Je?

Unaweza kupata habari zaidi kuhusu kujiunga na familia ya MMM kwa kubonyeza viunganisho viliyo hapa chini.

Associate MembersVolunteers | Prayer CircleSpecial Friends

 

Search...